N’na Kwetu
Mohammed Khelef Ghassani
* Affiliatelinks/Werbelinks
Links auf reinlesen.de sind sogenannte Affiliate-Links. Wenn du auf so einen Affiliate-Link klickst und über diesen Link einkaufst, bekommt reinlesen.de von dem betreffenden Online-Shop oder Anbieter eine Provision. Für dich verändert sich der Preis nicht.
Belletristik / Lyrik, Dramatik
Beschreibung
Hii ni riwaya ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya inayozu-ngumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kud-hibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC); na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighai ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya - na kung'oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifia ya Magharibi - na duniani kwa jumla. Ukisoma kitabu hiki utajiuliza, "mwandishi huyu aliwezaje kusuka riwaya inayoufanya moyo kukuenda mbio, hata kukulazimu wakati mwingine kukiweka kitabu kando ili urudishe pumzi! Ukishakianza tu, hutakiacha kabla ya kujua mwisho wa vita hi kali ya kimataifa. Na kivutio kikubwa ni kuwa kiongozi wa vita hiyo kwa upande wa Umoja wa Mataifa ni Murphy Ambilikile, Mtanzania - Willy Gamba wa Karne ya 21. Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa wasomaji wa riwaya za kiswahili.